Siro na Yohane

Mt. Siro katika mozaiki ya monasteri ya Hosios Lukas.

Siro na Yohane (alifariki Canopus, 31 Januari 311) ni wafiadini Wakristo wa Aleksandria (Misri) waliokatwa kichwa kwa imani yao.

Walikamatwa walipokwenda kuwatia moyo Teodosia, Teotista, Eudosia na mama yao Atanasia.

Kabla ya hapo, Siro alikuwa mganga, halafu mmonaki.

Habari zao ziliandikwa na patriarki Sofroni wa Yerusalemu.

Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 31 Januari[1].

  1. Martyrologium Romanum

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search